Krismasi nzuri!
Krismasi inasimama mbele ya mlango yetu, na baado tunahesabu siku chache mpaka inaanza mwaka mpia. Tunapenda kukumbuka juu ya mwaka 2015 na tunafurahi mwaka mpia 2016 italeta habari nyingi mbalimbali.
Sr. Christiana mwezi Agosti mwaka huu amechaguliwa kua Mama Mkuu ya Shirika ya Franziscan Sisters ya Maua, na anendelea badili ya Sr. Catherin ambaye alikuwa Mama Mkuu miaka sita.Tunatakia wote wawili kila ya heri na Baraka ya Mungu kwa kazi yao wanaofanya kwa shirika yenu.
Mivumoni ni mahali pazuri sana, hasa sababu ya Kwanza Project. Siku hizi wanamaliza kujenga internat ya shule nyumba ya kulala, na mensa, mahali pakula na jiko. Kutoka mwezi Januari 2016 Masista watafungua shule ya sekundari kwa wasichana. Watafika wanafunzi 50 wataishi ndani ya internat mpia. Sasa hivi wafanyakazi wanabidii sana kumaliza majengo ya shule, kabla wanafunzi wataingia Kwanza Project. Sisi tunafurahi sana wanafunzi wote wanapata nafasi kukaa ndani ya nyumba mpia ya kulala na kula. Sisi wote tunatakia Masista wote, mwalimu wote na Wanafunzi wote heri na baraka ya Mungu kuanza shule mpia ya sekundari.
Katika kilimo Masista na wanafunzi wanaweza sasa kuvuna , tuliootesha pamoja mwaka uliyopita. Zizini, ngombe wengi wanaendelea vizuri na hasa wanatoa faidi nyingi sana, nyama na maziwa, na shambani na bustanini wanapata mavuno mengi kwa kutegemea menyewe shuleni. „Kilimo kwanza, na kazi ya maendeleo.“
Sisi tunataka kusema asanteni sana kwa mojo, kwa wote waliyosaidia kwa njia ya fedha kwa shule yetu huko Mivumoni. Na shukrani pia kwa Masista wote wanayofanya kazi katika maendeleo ya shule, shambani ,bustanini na zizini.
Asanteni sana!
Sisi tunatakia heri na baraka ya mungu kwa Krismasi na mwaka mpia 2016.